ZITTO ATAKA TAMISEMI IMTAFUTE MWENYEKITI WA HALAMSHAURI ALIYETOWEKA


Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT -Wazalendo),Zitto Kabwe amemtaka waziri wa Tamisemi kulitafutia ufumbuzi suala la kutoweka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kakonko, Simon Kangue.
Amesema hayo bungeni jana Aprili 12,2018 alipochangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais,yenye wizara za Tamisemi,Utumishi na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
“Habari zinazosambaa Kibondo tayari ameuawa. Tunataka maelezo ya mtu huyo,sisi watu wa Kigoma ni Kigoma kwanza kabla ya kuwa Watanzania naomba hilo mlielewe,” amesema.
Zitto amesema mara ya mwisho kuonekana mwenyekiti huyo aliitwa kwa mkurugenzi na kukutana na ofisa usalama wa wilaya.
Amesema tangu siku hiyo hajulikani alipo mwenyekiti huyo licha ya jitihada za kumtafuta kufanyika.
“Familia imechukua hatua mbalimbali,imelalamika na sisi wajumbe wenzake tumehoji kwenye vikao,hakuna maelezo yoyote kutoka serikalini,”alisema Zitto.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA