Mh.George Simbachawene Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,George Simbachawene ameandika barua ya kujiudhulu wadhifa huo baada ya kutajwa katika ripoti za uchunguzi wa biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi iliyoonyesha namna serikali lilivyopoteza matrilioni ya fedha kutokana na sababu mbalimbali. Waziri Simbachawene ameandika barua hiyo muda mfupi baada ya Rais Magufuli kuwataka viongozi wote aliowateua na wametajwa katika ripoti hiyo wakae pembeni ili kupisha uchunguzi ambao utakuwa huru na wa haki. Mbali na Simbachawene,wengine waliokuwa wametakiwa kukaa pembeni ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Edwin Ngonyani ambaye alituhumiwa kutotekeleza majukumu yake kikamilifu alipokuwa akifanya kazi katika Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) lenye dhamana ya kusimamia madini. Mbali na Ngonyani,mwingine ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara,Eliakim Maswi baye naye amepaswa kupisha uchunguzi ambapo Rais ameagiza ufa...