NEEMA SEKTA YA AFYA-MKOANI RUKWA-Septemba 7,2017
Naibu waziri Suleiman Jafo |
Waziri Jafo ametoa majibu hayo leo bungeni mjini
Dodoma wakati akijibu maswali ya wabunge wa mkoani Rukwa waliotaka kujua mpango
wa serikali katika kuondoa changamoto mbalimbali zinazolenga sekta ya afya
Mkoani Rukwa na kuwa vikwazo kwa wananchi.
Miongoni mwa changamoto hizo ambazo ni kikwazo
kwa wananchi ni pamoja uhaba wa vituo
vya afya uhaba wa majengo na vyumba vya upasuaji katika hospitali.
Waziri Jafo amesema serikali imeelekeza nguvu
kujenga vyumba vya upasuaji katika kituo cha afya cha Kilando kilichopo
Halmashauri ya wilaya ya Nkasi huku akisema kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya
ya Kalambo ikitengewa shilingi Milioni 340 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya
Wilaya ya Kalambo.
Wakati huo huo amesema Halmashauri ya Wilaya ya
Sumbawanga ipo katika hali mbaya ambapo katika utatuzi wa upungufu wa vituo vya
huduma za afya serikali inaendelea kujenga Vituo vya afya vya Milepa na Mwimbe
ambapo imekwishapeleka shilingi zipatazo milioni 500 ili kuanza ujenzi na
uboreshaji.
Mkoa wa Rukwa unaundwa na Wilaya tatu ambazo ni
Sumabawanga Nkasi na Kalambo ambazo zinahitaji kuwepo kwa vituo vya huduma za
afya za kutosha katika Halmashauri 4 za mkoa huo ambazo ni Halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda,Halmashauri ya wilaya ya Mpanda,Nkasi na Kalambo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments