TUNDU LISSU APIGWA RISASI APELEKWA CHUMBA CHA UPASUAJI DODOMA-Septemba 7,2017
Mh.Tundu Lissu |
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi nyumbani kwake na kwamba
hali yake ni mbaya.
Lissu,ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chadema kwa sasa amepelekwa
chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, wabunge na viongozi
wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.
Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha
upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari, huku wengine wakilia.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Charles Kihologwe amewataka watu
hao kukaa mbali na chumba cha upasuaji lakini wengi wanakataa wakisema
hawamwamini mtu yeyote.
Asubuhi, Lissu alihudhuria kikao cha Bunge na aliomba mwongozo
wa Naibu Spika akihoji kuhusu taarifa za kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge,
Job Ndugai kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa
madini ya Tanzanite na almasi kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu badala ya kujadiliwa
na Bunge kwanza.
Habari zaidi ni www. p5tanzania.blogspot.com
Comments