TUMBUA TUMBUA VIGOGO WA SERIKALINI YABISHA HODI TENA-Septemba 7,2017



Rais Magufuli amewataka viongozi mbalimbali wa serikali ambao wametajwa kwenye ripoti za bunge ya madini ya Almasi na Tanzanite wamepishe nafasi zao ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake vizuri kuwachunguza.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akikabidhiwa ripoti hizo Ikulu jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kusema amesikia baadhi ya viongozi mbalimbali wengine ambao amewateuwa yeye kuwa wameusishwa kwenye wizi huo hivyo amewataka wapishe.
"Wako watu wametajwa tajwa, na wengine mimi ndio nilihusika kuwateua sasa ukishatajwa tajwa, naagiza vyombo vya ulinzi na usalama vifuatilie hili tena kwa haraka.
" Wale ambao wametajwa tajwa kwenye ripoti hii ambao ni wateule wangu, ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake vizuri, ni matumaini yangu watakaa pembeni" alisema Rais Magufuli
Katika ripoti hiyo ambayo iliwasilishwa jana mjini Dodoma na leo kukabidhiwa kwa Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa iliweza kuwataja baadhi ya viongozi wa serikali ikiwepo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh.George Simbachawene, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA