EKARI 100 ZATENGWA MKOANI RUKWA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA-Septemba 7,2017
Aliyesimama ni Mh.Bupe Mwakang'ata |
Kwa
sasa taratibu za ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi huo zinakamilika
na serikali itawalipa fidia stahiki wahusika.
Akijibu
swali bungeni leo,Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Seleman
Jafo amesema kwa sasa wagonjwa wanapata huduma katika hospitali teule
iliyopo pamoja na vituo vya Afya na zahanati.
Katika
swali la msingi, mbunge wa viti maalumu Bupe Mwakang'ata (Chadema),
ametaka kujua ni lini serikali itajenga hospitali ya wilaya katika wilaya
za Nkasi na Sumbawanga ambako wanawake wanapata shida.
"Serikali
itajitahidi kutafuta fedha na kushirikiana na wananchi wa Nkasi ili kufanikisha
ujenzi wa hospitali ya wilaya," amesema Jafo.
Kuhusu
hospitali ya rufaa alisema Mkoa wa Rukwa umeanza taratibu za ujenzi wa
hospitali katika eneo la Milanzi ambapo hospitali inayotumika kwa sasa itabaki
kuwa hospitali ya wilaya ya Sumbawanga.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments