WAZIRI SIMBACHAWENE AJIUDHULU KWA AGIZO LA RAIS MAGUFULI-Septemba 7,2017
Mh.George Simbachawene |
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,George Simbachawene
ameandika barua ya kujiudhulu wadhifa huo baada ya kutajwa katika ripoti za
uchunguzi wa biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi iliyoonyesha namna
serikali lilivyopoteza matrilioni ya fedha kutokana na sababu mbalimbali.
Waziri
Simbachawene ameandika barua hiyo muda mfupi baada ya Rais Magufuli kuwataka
viongozi wote aliowateua na wametajwa katika ripoti hiyo wakae pembeni ili
kupisha uchunguzi ambao utakuwa huru na wa haki.
Mbali
na Simbachawene,wengine waliokuwa wametakiwa kukaa pembeni ni Naibu Waziri wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Edwin Ngonyani ambaye alituhumiwa
kutotekeleza majukumu yake kikamilifu alipokuwa akifanya kazi katika Shirika la
Madini la Taifa (STAMICO) lenye dhamana ya kusimamia madini.
Mbali
na Ngonyani,mwingine ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara,Eliakim Maswi baye naye
amepaswa kupisha uchunguzi ambapo Rais ameagiza ufanywe na vyombo vya ulinzi na
usalama haraka iwezekanavyo.
Rais
Dkt Magufuli ametoa maagizo hayo leo alipokuwa akipokea ripoti hiyo ya
uchunguzi wa madini kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye aliipokea
jana kutoka katika kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Rais
Magufuli aliviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi kwa wateule
wake waliotajwa tajwa katika ripoti hizo lakini akasema kuwa,uchunguzi hauwezi
kufanyika wakati kiongozi akiwa bado yupo serikali.
Baada
ya kusema hivyo,Rais Magufuli alisema anaamini kuwa viongozi hao watakaa
pembeni kupisha uchunguzi.
Hafla
hiyo ya kukabidhi ripoti ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Job Ndugai,Wenyeviti wa kamati mbili za
Tanzanite na Almasi, Dotto Biteko na Mussa Azzan Zungu ambao wote ni wabunge.
Wengine
waliohudhuria ni pamoja na viongozi mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama,
viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa jumuiya ya wanafunzi wa elimu ya juu
pamoja na viongozi waandamizi wa serikali.
Rais
Magufuli ameendelea kuwasisitiza watanzania kuwa wazalendo kwani rasilimali za
nchi kwani rasilimali zinaibiwa na watanzania kuendlea kubaki katika umasikini
uliokithiri.
Baada
ya kuhutubia, Rais Magufuli alikabidhia nakala za ripoti hiyo kwa viongozi wa
vyombo vya ulinzi na usalama ili vianze kufanya kazi mara moja na sio kuendelea
kukaa huku mali za watanzania zikiibiwa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments