Posts

Showing posts from August 2, 2017

WAHAMIAJI HARAMU WILAYANI MLELE MKOANI KATAVI KUANZA KUSAKWA-Agosti 2,2017

Mkuu wa wilaya ya mlele mkoani Katavi Rahel Kasanda amewaagiza watendaji wa idara mbalimbali kataka Halmashauri hiyo kushirikiana vema na wananchi katika kuwabaini wahamiaji haramu wanaoingia katika wilaya hiyo. 

WAKAZI MANISPAA YA MPANDA WAUNGA MKONO DAWA ZA CHANJO KWA WATOTO ZICHUNGUZWE KUTOKANA NA WATOTO KULEWA,KUANGUKA NA KUZIMIA WANAPOTUMIA DAWA HIZO-Agosti 2,2017

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameunga mkono hoja ya baadhi ya madiwani waliotaka ziangaliwe upya dawa za chanjo zinazosababisha wanafunzi wa shule za msingi kuanguka na kuzimia baada ya kunywa dawa hizo.

WIKI YA UNYONYESHAJI DUNIANI YAANZA,WAZAZI KATAVI WAASWA KUNYONYESHA KWA MUDA WA KUTOSHA KWA AJILI YA AFYA ZA WATOTO-Agosti 2,2017

Ikiwa ni wiki ya unyonyeshaji duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo mwezi wa nane,wazazi  mkoani Katavi  wametakiwa kuwanyonyesha watoto mpaka wafikiapo umri wa miaka miwili ili kulinda afya zao.  Muuguzi wa kituo cha afya cha Town Clinic katika halmashauri ya  Manispaa ya Mpanda Mkoani  Katavi Lugalata Elias amesema  ikiwa ni wiki ya unyonyeshaji maziwa,  wazazi wanatakiwa kufuata ushauri wanaopewa na watoa  huduma ili kuepuka kudhoofika kwa afya ya mtoto.