WIKI YA UNYONYESHAJI DUNIANI YAANZA,WAZAZI KATAVI WAASWA KUNYONYESHA KWA MUDA WA KUTOSHA KWA AJILI YA AFYA ZA WATOTO-Agosti 2,2017
Ikiwa ni wiki ya unyonyeshaji duniani ambayo
huadhimishwa kila mwaka ifikapo mwezi wa nane,wazazi mkoani Katavi wametakiwa kuwanyonyesha watoto mpaka
wafikiapo umri wa miaka miwili ili kulinda afya zao.
Muuguzi wa kituo cha afya cha Town Clinic katika halmashauri
ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Lugalata Elias amesema ikiwa ni wiki ya unyonyeshaji maziwa, wazazi wanatakiwa kufuata ushauri wanaopewa na
watoa huduma ili kuepuka kudhoofika kwa
afya ya mtoto.
Aidha ameongeza kuwa kutokana na kutofata ushauri wanaopewa na watoa huduma hupelekea
madhara kwa mtoto ikiwa ni pamoja na kudumaa, kupungua kilo pamoja na kupata ugonjwa
wa kilibatumbo.
Kwa upande wa wazazi wameeleza kuwa kutowanyonyesha
watoto kwa wakati au kuwaachisha mapema, ni kutokana na
mazingira magumu wanayopitia katika kipindi cha unyonyeshaji.
Habarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments