ZIMAMOTO MKOANI KATAVI NYUMBA KWA NYUMBA KUEPUSHA HATARI-Septemba 6,2017
JESHI la zimamoto na uokoaji mkoani Katavi limesema linaanza oparesheni ya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba kubaini watu wenye tabia ya kuchimba vyoo au visima na kuacha bila kufukia mashimo hayo hali ambayo husababisha vifo vya watu wanapokuwa wametumbukia katika mashimo hayo.