TAARIFA MPYA KUHUSU UCHAGUZI WA KENYA-Septemba 6,2017
Baada ya kiongozi wa upinzani
Kenya Raila Odinga kutangaza kutoshiriki katika marudio ya Uchaguzi Mkuu mpaka
Tume ya Uchaguzi ifanyiwe mabadiliko, sasa good news kwake ni kwamba, Tume hiyo
imetangaza kundi la watu sita ambalo litasimamia uchaguzi huo.
Walioteuliwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Ezra Chiloba, Naibu wake Betty Nyabuto, Mkurugenzi wa Usajili wa wapiga kura pamoja na Mkuu wa Operesheni za Uchaguzi Immaculate Kasait, Naibu wake Mwaura Kamwati, Mkuu wa Operesheni za Tume na Mkuu wa Teknolojia James Muhati.
Uchaguzi wa marudio Kenya
umepangwa kufanyika October 17, 2017 kutokana na ruhusa ya Mahakama ya Juu
nchini humo kufuatia kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na Odinga.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments