LEO WANAFUNZI WA DARASA LA SABA WANAANZA KUFANYA MTIHANI WA KUHITIMU ELIMU YA MSINGI-Septemba 6,2017
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde |
Wanafunzi 917,072 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu
ya msingi leo na kesho (Septemba 7).
Kati ya wanafunzi hao, wavulana ni 432,744 sawa na asilimia
47.19, wakati wasichana ni 484,328 sawa na asilimia 52.81.
Watahiniwa 882,249 watafanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili
na 34,823 watatumia lugha ya Kiingereza.
Jumla ya watahiniwa 94 wasioona wamesajiliwa kufanya
mtihani huo, wakiwemo wavulana 58 na wasichana 36.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta),
Dk Charles Msonde amesema maandalizi yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa
kwa vifaa vinavyohitajika katika halmashauri zote nchini.
‘’Dk Msonde amezitaka
halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa mitihani unazingatiwa.’’
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments