VIONGOZI WANNE WA CUF WANAMUUNGA MKONO WAFARIKI DUNIA-Septemba 6,2017
Habari zilizotufikia
hivi punde ni kwamba Viongozi wanne wa Chama cha Wananchi CUF wanaomuunga mkono
Profesa Ibrahim Lipumba wamefariki dunia baada ya msafara wao kupata ajali
maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani.
Ajali
hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo wakati Viongozi hao wakitokea Dodoma kwenye
sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho baada ya gari lao
kugongana na Lori.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa CUF Abdallah Kambaya Viongozi
waliofariki ni kutoka Wilaya ya Muheza, Tanga ambapo miongoni mwao ni Mgombea
Udiwani wa Muheza Mjini, aliyefahamika kwa jina la Uredi.
Hata
hivyo idadi ya majeruhi haijajulikana ila hawazidi 10 na baadhi yao wapo
Hospital ya Tumbi huku akisema chanzo cha ajali hiyo ni gari la wafuasi hao
kugongana na lori.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments