MADAKTARI 25 WAGOMEA AJIRA ZA RAIS MAGUFULI-Septemba 6,2017
Madktari 25 kati ya 258 wa Tanzania ambao
walikidhi vigezo vya kwenda kufanyakazi Kenya wamekataa ajira zilizotolewa na
Rais Magufuli kuwa wafanye kazi hapahapa nchini kutokana na safari yao ya Kenya
kuhairishwa.
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk
Obadia Nyongole amesema baadhi ya madaktari waliopaswa kuajiriwa nchini
wamekwenda kinyume na viapo vya madaktari vinavyowataka kuweka mbele utoaji
huduma na sio maslahi kama wanavyofanya wao kwa kuonesha tamaa za kwenda kenya
ili kupata mshahara mkubwa.
Dk. Obadia alisema kuwa, madaktari hao 25
wamekataa kuajiriwa na serikali, wakisema kama wangekwenda nje ya nchi basi
wangepata malipo mazuri kuliko ambayo watalipwa endapo watakubali kufanya kazi
nchini.
Uamuzi wa kuwaajiri madaktari hao 258 nchini
Tanzania badala ya Kenya ulitangazwa mwezi Aprili na Waziri wa Afya, Ummy
Mwalimu kutokana na kutetereka kwa makubalino ya serikali ya Tanzania na
Kenya kufuatia Mahakama nchini, Kenya kutoondoa pingamizi lililofunguliwa
kuhusu ajira za madaktari wa Tanzania nchini humo.
“Rais Magufuli ameamua kuwa, madaktari hao 258 ambao walikuwa
tayari kwenda kufanya kazi nchini Kenya waajiriwe serikalini mara moja.”
Mnamo mwezi machi 18, mwaka huu, Rais Magufuli
alisema, Tanzania imekubali ombi la kuipa Kenya madaktari 500
watakaoisaidia nchi hiyo kukabiliana na tatizo la uhaba wa madaktari na mgomo
wa madaktari nchini humo.
“Matatizo ya Kenya ni matatizo ya Tanzania, tutawapatia
madaktari hao 500 ili wakatoe huduma ya matibabu kwa ndugu zetu waliopo Kenya,
na kwa kuwa mmenihakikishia kuwa madaktari wangu mtawalipa mishahara
inavyotakiwa, mtawapa nyumba za kuishi, na mtahakikisha wanafanya kazi katika
mazingira mazuri na salama mimi sina tatizo na naamini mambo yatakwenda vizuri,” alisema Rais
Magufuli.
Kwa mujibu wa Dk. Obadia, serikali hutumia
kati ya Tsh 60 milioni hadi Tsh 90 milioni kumsomesha daktari mmoja na hutoa
ruzuku au mikopo ya bei nafuu kwa watu wanaosomea taaluma ya udaktari kwa
tegemeo kuwa baada ya kuhitimu warudi kuja kuhudumia raia waliopo nchini kwao
kwalengo la kuisaidia nchi yao.
Agosti 16,mwaka huu serikali kupitia kwa Waziri wa Afya
maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu alisema Mgao wa
madaktari hao 258 waliotakiwa kwenda nchini Kenya kufanya kazi,kati yao madaktari
5 walelezwa kuletwa Mkoani Katavi ambapo Manispaa ya Mpanda ilipokea-watumishi
3,Halmashauri ya Nsimbo mtumishi -1 huku mpaka kufika Agosti 16 ya mwaka huu
ripoti ya waziri ilionesha mtumishi aliyekuwa amepangiwa Halmashauri ya wilaya
ya Mlele alikuwa hajaripoti.
Hata hivyo serikali ilitangaza kuajiri watumishi wa sekta ya
Afya 3100 wakiwemo 35 katika Halamshauri tano za Mkoani Katavi kabla ya
Septemba 30 mwaka huu.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments