ZIMAMOTO MKOANI KATAVI NYUMBA KWA NYUMBA KUEPUSHA HATARI-Septemba 6,2017
JESHI la zimamoto na uokoaji mkoani
Katavi limesema linaanza oparesheni ya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba kubaini watu wenye tabia ya kuchimba vyoo au
visima na kuacha bila kufukia mashimo
hayo hali ambayo husababisha vifo vya
watu wanapokuwa wametumbukia katika mashimo hayo.
Mkuu wa Ukaguzi wa Jeshi la Zima moto
Koplo Wilfred Ruhega amesema mwananchi
atakayeshindwa kutii sheria bila shurti hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi yake.
Ameongeza kuwa zoezi hilo la ukaguzi
unaofanywa kwenye majengo pamoja na vyombo vya usafiri unaenda sambamba na tozo
ambazo zipo tofauti kulingana na eneo husika.
Jeshi hilo linatoa kauli hiyo ikiwa
ni kutoa mwongozo kwa wananchi ambao wamekuwa wakitoa taarifa kwa jeshi la
polisi kwa kutokujua kwa kuwa majanga yote kama hayo yapo chini ya jeshi hili
lililo chini ya Wizara ya Mambo ya ndani nchi.
Kwa upande wake Kopro Pastori
Stanslaus Skwara Mthamini wa jeshi hilo mkoani katavi amesema viwango
tofautitofauti vilivyoainishwa
vimepangwa kwa mujibu wa sheria hivyo ni vema wananchi kutii sheria bila shuruti.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments