Posts

Showing posts from December 8, 2017

MKOA WA RUKWA UMESHAULIWA KUONGEZA VITUO VYA HUDMA ZA AFYA

MKOA wa Rukwa umeshauriwa Kuongeza vituo vya kutolea huduma za afya ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa unaoendelea kuongezeka siku hadi siku kutokana na ongezeko la watu. Naibu waziri wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Josephat Kandege alitoa ushauri huo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na uongozi wa mkoa huo wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi. Alisema kuwa hivi sasa mkoa huo unaidadi kubwa ya watu hali iliyosababisha kuwepo idadi kubwa ya wagonjwa katika maeneo ya kutolea huduma za afya hivyo nilazima mkakati wakujenga zahanati, vituo vya afya na hospitali uanze mara moja ilikuendana na idadi ya wakazi wa mkoa huo.  Waziri Kandege alisema kuwa fursa nyingine iliyopo ni kuyatumia majengo yanayo achwa na makampuni ya kigeni ya ujenzi wa barabara mkoani humo kwani yakibadilishwa na kuboreshwa yanaweza kufaa kutumika kutolea huduma za afya.  Alisema kuwa zipo baadhi ya wilaya hazina hospitali ni vizuri sasa zikajipanga kujenga ili kuwafikis...

UHABA WA WATUMISHI VITUO VYA AFYA UVINZA NA NGURUKA MKOANI KIGOMA.

VITUO vya afya Uvinza na Nguruka vilivyopo wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma vinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa watumishi katika kada zote na hivyo kuathiri ufanisi wakazi ambao unaweza kusababisha vifo kwa wagonjwa wanaohitaji huduma katika vituo hivyo. Zena Shaban na Mapinduzi Hamisi ni baadhi ya wananchi katika wilaya ya uvinza ambapo wameiamba mpanda redio kero wanazo kumbana nazo na mapendekezo yao kwa serikali. Stanford Chamgeni ambaye ni mganga mfawidhi wa kituo cha afya Nguruka amesema wanakumbana na kazi kubwa wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa ambapo kwa siku hutoa huduma kwa wagonjwa 80 hadi 100 huku mganga wa Kituo cha afya Uvinza Albert Msingwa akielezea upungufu wa majengo katika kituo chake. Naye Mganga mkuu wa Wilaya hiyo Albert Mumwi amekiri mapungufu hayo na kuelezea kuwa kufikikia sasa tayari wauguzi 10 wamepatiwa ajila na tayari wamepangiwa vituo vya kazi. Tatizo hilo la upungufu wa watumishi limetajwa kuwa kero ya muda mrefu kati...

MKOANI KATAVI AHUKUMIWA JELA MIAKA 20 BAADA YA KUKAMATWA NA NYAMA YA KIBOKO KILO 110

Mahakama ya Wilaya ya Mpanda imemuhukumu Omary Maganga (45) kutumikia jela kifungo cha miaka 20 baada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na nyama ya kiboko zaidi ya kilo 110. Hukumu hiyo Imetolewa leo Ijumaa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda,Chiganga Tengwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka uliokuwa ukiongozwa na mwa nasheria wa Serikali, Flaviani Shio. Awali,katika kesi hiyo mwendesha mashitaka huyo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Maganga alitenda kosa hilo Oktoba 10 mwaka 2016 nyakati za saa 10 jioni. Alidai kuwa siku ya tukio mshitakiwa alikamatwa akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi huku akiwa na nyama ya kiboko yenye uzito wa kilo 118 ambayo thamani yake Sh 3.2 milioni. Mwanasheria huyo wa Serikali ameiambia mahakama kuwa mshitakiwa huyo alikamatwa na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi baada ya kuwa wamepata taarifa kutoka kwa raia wema za kuwa mshitakiwa amekuwa akifanya ujangili kwen...

DC MPANDA ATAKA JAMII KUACHANA NA MILA KANDAMIZI KWA WANAWAKE NA WATOTO

Na.Issack Gerald Mkuu wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Bi.Lilian Charles Matinga ameitaka Jamii kuachana na mila kandamizi dhidi ya wanawake na watoto wa kike. Bi.Matinga ametoa kauli hiyo katika kilele cha siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya mtoto wa kike na mwanamke.  Baadhi ya wanawake katika kilele hicho wameelezea mimba za utotoni kuwa changamoto katika maendeleo kwa vizazi vi javyo. Aidha wametaja nafasi ndogo ya ushiriki wa wanawake katika maamuzi ndani ya familia husababisha kuendelea kwa dhuruma dhidi ya makundi ya wanawake. Maadhimisho hayo yamefanyika katika kijiji cha ivungwe,kata ya katumba halamsahuri ya nsimbo yakiwa na kauli isemyo Funguka ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto haumuachi mtu salama chukua hatua. Katika kipindi cha Mwezi Januari mpaka Juni mwaka 2017 jumla ya wanafunzi 14 wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo waliripotiwa kupata ujauzito hali ambayo ilichukuliwa kama ukatiri wa kijinsia. Habari zaidi ni P5...

JESHI LA POLISI MKOANI PWANI BADO HALINA TAARIFA ZA KUWEZESHA KUPATIKANA MWANDISHI WA HABARI ALIYEPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA

Na.Issack Gerald Jeshi la Polisi Mkoani Pwani limesema mpaka sasa halina taarifa za kutosha zinazowezesha kupatikana mwandishi wa gazeti la mwananchi Azori Gwanda aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha siku 18 zilizopita. Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa Jeshi hilo Mkoani Pwani Kashmishna Msaidizi Jonathani Shana ambapo amewataka wananc hi wenye taarifa muhimu kuhusu tukio hilo walitaarifu jeshi la polisi ili lizifanyie kazi. Katika hatua nyingine,Kamanda Shana amesema siyo miili yote ilioonekana ikielezea katika habari ya hindi miezi michache iliyopita inahusishwa na utekaji bali pia imebainika hata matukio ya ajali,upepo na uzembe wa baadhi ya wahanga vinahusika. Mkoa wa Pwani ni Mkoa ambao umekubwa na matukio watu kupigwa risasi na kuuwawa na watu wasiojulikana wakiwemo viongozi wa serikali za mitaa na maafisa wa polisi hali ambayo imesababishwa kuanzishwa mkoa wa kipolisi Mkoani Pwani kama njia mojawapo ya kudhibiti matukio hayo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMIT...

MANISPAA YA MPANDA KUADHIMISHA MIAKA 56 UHURU WA TANZANIA BARA KWA KUFANYA USAFI.

Na.Issack Gerald Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi inatarajia kuadhimisha miaka 56 ya uhuru wa Tanzania bara kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Manispaa. Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu ametaja miongoni mwa maeneo yatakayofanyiwa usafi kwa kushirikisha watumishi wa umma ni pamoja na maeneo ya stendi,Hospitali na maeneo ya soko. Aidha Nzyungu ame wataka wananchi wote kushiriki ipasavyo katika kaufanya usafi katika maeneo yao ili kuweka mazingira katika hali ya usafi. Kwa mjibu wa Bw.Nzyungu zoezi la usafi la kesho katika maeneo yote ya Mkoa wa Katavi linaratibiwa na uongozi wa Mkoa wa Katavi. Hatua ya kufanya usafi siku ya kesho ni utekelezaji wa agizo la rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt John Magufuli ambaye miaka miwili iliyopita aliagiza siku ya jumamosi itumike kwa ajili ya usafi nchi nzima. Tanganyika(Tanzania bara) ilipata uhuru kutoka kwa Uingereza Demba 9 mwaka 1961 chini ya Rais wa Kwanza wa Tanganyik...

ZAIDI YA MADEREVA 300 WA PIKIPIKI WILAYANI MPANDA WAMEHITIMU MAFUNZO

Na.Issack Gerald Madereva pikipiki maarufu kama bodaboda mjini Mpanda wameishukuru mamlaka inayosimamia usafiri wa nchi kavu na majini nchini (SUMATRA) kwa kufanikisha mafunzo ya udereva kwa madereva hao . Mwenyekiti wa Bodaboda Mjini Mpanda Stefano Mwakabafu amesema mafunzo hayo yameendeshwa na chuo cha VETA Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya uvikama kwa hisani ya SUMATRA mkoa wa  katavi. Katika hatua nyingine amewaomba wadau wengine kujitokeza kufadhili mafunzo kama hayo katika wilaya zingine za mkoa wa Katavi ili vijana wengi waendelee kujiajiri kupitia kazi ya udereva piki piki. Mafunzo hayo ya siku tatu yamehitimshwa ambapo zaidi ya madereva 300 wamehudhuria mafunzo ambayo yamefanyikia katika shule ya msingi Azimio ilipo Manispaa ya Mpanda. Mafunzo yalihitimishwa Desemba 5 mwaka huu yakilenga kuwapatia mafunzo ya matumizi sahihi ya pikpiki na uzingatiaji wa sheria na alama za uslama barabarani. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WANANCHI MKOANI KATAVI WAZUNGUMZIA MIAKA 56 YA UHURU WA TANGANYIKA

Baadhi ya wananchi mkoani katavi wameeleza mafanikio katika miaka 56 ya uhuru wa Tanzania ambapo wamemeelezea kupiga hatua kimaendeleo katika sekta mbalimbali. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema maendeleo yaliyopo tangu uhuru ni pamoja na kimarika kwa miundo mbinu kama vile barabara na uimarishaji wa huduma za kijamii. Aidha wameongeza kuwa kuna maendeleo makubwa katika Nyanja za mawasiliano hali in ayopelekea kukua kiuchumi tofauti na miaka ya nyuma ambapo mawasiliano ilikuwa kwa njia ya barua pekee. Maadhimisho ya Miaka 56 ya uhuru wa Tanzania bara yatafanyika disemba 9 mwaka huu uwanja wa jamuhuri mjini Dodoma kauli mbiu ni uhuru wetu ni tunu,tuudumishe, tuulinde,tukemee rushwa na uzembe. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

KIJIJI CHA MTAMBO WILAYANI MPANDA CHATOKOMEZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO

Na.Issack Gerald Kijiji cha Mtambo kilichopo kata ya Katumba Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,kimefanikiwa kutokomeza vifo vya akina mama na watoto. Hatua hiyo imethibitishwa na Katibu wa Kijiji cha Mtambo Bw.Fenias Fulujensi wakati akijibu malalamiko ya baadhi ya wananchi wanaolalamika kutozwa faini ya shilingi elfu ishirini kutoka kwa wananchi ambao wake zao wanaojifungulia nyumbani. Bw.Fulujensi amesema kati ka kipindi cha mwaka 2016 mpaka 2017 wanawake watatu wamefariki dunia kutokana na kuchelewa kufika katika vituo vya huduma za afya ambapo kwa sasa hakuna ripoti ya vifo hivyo. Hata hivyo Kamimu afisa mtendaji wa Kata ya Katumba Bi.Lucy Kagine ameunga mkono faini hiyo japo amesema hana taarifa ya uwepo wa faini hiyo katika kijiji hicho. Kwa mjibu wa mwenyekiti wa Kamati ya zahanati ya kijiji cha Mtambo Bw.Karoli Shaltiel amesema kwa kushirikiana na Halmashauri ya serikali ya kijiji cha Mtambo imechukua hatua ya kutunga sheria ndogondogo za kutoza faini baada ya kuoneka...

SOKO KUU LA VYAKULA WILAYANI MLELE KUONDOLEWA KATIKATI YA MJI

Soko kuu la vyakula lililopo katikati ya mji wa Inyonga katika halmashauri ya wilaya ya mlele mkoa wa katavi linatarajiwa kuhamishiwa katika eneo la kalovya lililopo katika halimashauri hiyo. Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Mlele Rachel Kasanda wakati akizungumza na wafanya biashara wa wilaya hiyo kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Inyonga. Katika kikao hicho mkuu   huyo wa wilaya pamoja na mkurugenzi mtendaji wa halimashauri hiyo Alexius Kagunze kwa pamoja wamechangia mifuko kumi ya simenti kila mmoja. Wakati huo huo wafanya biashara wa soko hilo wakiuunga mkono jitihada hizo kwa kuahidi kutoa michango mbali mbali. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WILAYA YA MPANDA IMETENGA HEKA ZAIDI YA 7000 KWA AJILI YA WALIOONDOLEWA KATIKA MAENEO YA HIFADHI

Na.Issack Gerald Mkuu wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Lilian Matinga amesema zaidi ya heka elfu saba zimetengwa kwa ajili ya wananchi walioondolewa katika maeneo ya hifadhi za misitu.  Bi.Matinga amesema kitendo cha uvamizi wa misitu ni uhalifu na kwamba kila mwananchi anapaswa kuishi mahali popote kwa kufuata sheria. Katika hatua nyingine amewaonya baadhi ya viongozi wanao waru buni wananchi ili kuyarudia maeneo hayo kuacha maramoja na kuwatadharisha kuwa sheria itachukua mkondo wake. Awali baadhi ya viongozi wa kata ya Stalike ambayo vitongoji vyake vimekumbwa na sakata hilo wamekana kuwepo kwa maeneo yaliyotengwa kwaajili ya wananchi hao ambao wanaishi porini. Sanjari na hayo viongozi hao wameshutumiwa na wananchi kwa kitendo cha kuwachangisha fedha kwa madai ya kutaka kuonana na waziri Mkuu ili kulipatia ufumbuzi suala hilo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

VIBAKA WATISHIA USALAMA KWA WAKAZI WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI

Na.Issack Gerald Baadhi ya Wananchi kata ya Misukumilo Manispaa ya Mpanda wamedai kuingiwa na hofu kufuatia kukithiri kwa matukio ya kiharifu katika eneo la linalofahamika kwa jina la Migazini. Wakazi hao wamesema vitendo vya kiharifu katika eneo la migazini vimekithiri na hivyo kuliomba jeshi la polisi kushughulikia tatizo hilo. Wametaja uporaji wa mali za nyumbani na kukabwa njiani kasha kunyang’anywa mali n i miongoni mwa matukio yanayofanywa na vibaka hao. Afisa mtendaji wa kata hiyo Pasca Mbete amekili kuwepo kwa vitendo hivyo na kuahidi kuimarisha ulinzi na usalama ili kuondoa adha hiyo. Kwa upande wa Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Katavi Damasi Nyanda amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kuwabaini waharifu hao. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

SUMATRA MKOANI KATAVI IMETOA ANGALIZO UPANDISHAJI HOLELA WA NAULI MSIMU WA SIKUKUU.

Na.Issack Gerald Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi,imewataka wamiliki na wasafirishaji wa vyombo vya moto Mkoani Katavi kutopandisha nauli kiholela katika msimu wa sikukuu. Kauli hiyo imetolewa na Afisa Sumtra Mkoani Katavi Bw.Amani Mwakalebela ambapo amesema watakaopandisha nauli bila kibali watachukuliwa hatua za kisheria. Mwakalebela amebainisha  kuwa miongoni mwa sehemu zinazolalamikiwa ni pamoja na barabara kutoka Mpanda mpaka Inyonga Wilayani Mlele ambapo mamlaka hiyo imesema inatarajia kubandika viwango vya nauli katika stendi ili kuondoa malalamiko kuhusu nauli huku wasafiri wakitakiwa kuripoti matukio ya kutozwa nauli zisizo halali. Kumekuwa na baadhi ya wasfairishaji wa vyomvo vya moto kujipandishia nauli kiholela ambapo hatua hiyo imepongezwa na baadhi ya wananchi wakisema inalenga usawa kati ya wenye vyombo vya usafiri na abiria. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

VIKUNDI ZAIDI YA 40 VYA WAJASILIAMALI WAJANE MKOANI KATAVI VIMEZINDULIWA,MBUNGE AVIPATIA MTAJI WA KIANZIO

Na.Issack Gerald Mbunge wa viti maalumu mkoani Katavi Taska Mbogo(CCM) amewataka wanawake kujiunga katika vikundi mbalimbali ili wapatiwe mikopo itakayowasaidia kumudu hali ngumu ya kimaisha. Mbogo ametoa wito huo wakati akizindua vikundi cha wajasiriamali vya wakina mama wajane zaidi ya 40 kutoka mitaa ya msasani,tambuka reli na mpanda hoteli. Katika uzinduzi huo amega wa mtaji wa gunia tatu za mchele na pesa zaidi ya shilingi laki moja kwa ajili ya kusajili vikundi vyao. Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake CCM(UWT) kata ya mpanda hoteli Bi.Elika George ambaye ni miongoni mwa wanakikundi hao amesema kujiunga katika vikundi hivyo kutawasaidia kujikwamua kimaisha na kuondokana na hali ya kuwa omba omba. Bi.George amewashauri akina mama wenzake kujikita zaidi katika malengo ya shghuli zitakazowakwamuakiuchumi. Kwa upande wao akina mama mbali na kumshukuru mbunge kwa mchango wake wamesema watadhititi vema kutumia mtaji huo katika kujiendeleza ili waondokane na umaskini. Kuundwa...