SUMATRA MKOANI KATAVI IMETOA ANGALIZO UPANDISHAJI HOLELA WA NAULI MSIMU WA SIKUKUU.

Na.Issack Gerald

Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi,imewataka wamiliki na wasafirishaji wa vyombo vya moto Mkoani Katavi kutopandisha nauli kiholela katika msimu wa sikukuu.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Sumtra Mkoani Katavi Bw.Amani Mwakalebela ambapo amesema watakaopandisha nauli bila kibali watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwakalebela amebainisha kuwa miongoni mwa sehemu zinazolalamikiwa ni pamoja na barabara kutoka Mpanda mpaka Inyonga Wilayani Mlele ambapo mamlaka hiyo imesema inatarajia kubandika viwango vya nauli katika stendi ili kuondoa malalamiko kuhusu nauli huku wasafiri wakitakiwa kuripoti matukio ya kutozwa nauli zisizo halali.

Kumekuwa na baadhi ya wasfairishaji wa vyomvo vya moto kujipandishia nauli kiholela ambapo hatua hiyo imepongezwa na baadhi ya wananchi wakisema inalenga usawa kati ya wenye vyombo vya usafiri na abiria.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA