ZAIDI YA MADEREVA 300 WA PIKIPIKI WILAYANI MPANDA WAMEHITIMU MAFUNZO
Na.Issack Gerald
Madereva pikipiki maarufu kama bodaboda mjini
Mpanda wameishukuru mamlaka inayosimamia usafiri wa nchi kavu na majini nchini
(SUMATRA) kwa kufanikisha mafunzo ya udereva kwa madereva hao.
Mwenyekiti wa Bodaboda Mjini Mpanda Stefano
Mwakabafu amesema mafunzo hayo yameendeshwa na chuo cha VETA Mkoa wa Katavi kwa
kushirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya uvikama kwa hisani ya SUMATRA mkoa
wa katavi.
Katika
hatua nyingine amewaomba wadau wengine kujitokeza kufadhili mafunzo kama hayo
katika wilaya zingine za mkoa wa Katavi ili vijana wengi waendelee kujiajiri
kupitia kazi ya udereva piki piki.
Mafunzo
hayo ya siku tatu yamehitimshwa ambapo zaidi ya madereva 300 wamehudhuria
mafunzo ambayo yamefanyikia katika shule ya msingi Azimio ilipo Manispaa ya
Mpanda.
Mafunzo
yalihitimishwa Desemba 5 mwaka huu yakilenga kuwapatia mafunzo ya matumizi
sahihi ya pikpiki na uzingatiaji wa sheria na alama za uslama barabarani.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments