KIJIJI CHA MTAMBO WILAYANI MPANDA CHATOKOMEZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO
Na.Issack Gerald
Kijiji cha Mtambo kilichopo kata ya Katumba
Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,kimefanikiwa kutokomeza vifo vya akina mama na
watoto.
Hatua hiyo imethibitishwa na Katibu wa Kijiji
cha Mtambo Bw.Fenias Fulujensi wakati akijibu malalamiko ya baadhi ya wananchi
wanaolalamika kutozwa faini ya shilingi elfu ishirini kutoka kwa wananchi ambao
wake zao wanaojifungulia nyumbani.
Bw.Fulujensi amesema katika kipindi cha mwaka 2016 mpaka 2017 wanawake watatu wamefariki dunia
kutokana na kuchelewa kufika katika vituo vya huduma za afya ambapo kwa sasa
hakuna ripoti ya vifo hivyo.
Hata hivyo
Kamimu afisa mtendaji wa Kata ya Katumba Bi.Lucy Kagine ameunga mkono faini
hiyo japo amesema hana taarifa ya uwepo wa faini hiyo katika kijiji hicho.
Kwa mjibu
wa mwenyekiti wa Kamati ya zahanati ya kijiji cha Mtambo Bw.Karoli Shaltiel
amesema kwa kushirikiana na Halmashauri ya serikali ya kijiji cha Mtambo
imechukua hatua ya kutunga sheria ndogondogo za kutoza faini baada ya kuonekana
asilimia 60 ya akina mama wanajifungulia nyumani hali ambayo imesababisha vifo
kwa mama na mtoto.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments