HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA
Lazaro Nyalandu alizaliwa
Agosti 18, 1970 mkoani Singida, hivyo atafikisha miaka 45 Agosti mwaka huu. Kwa
sasa yeye ni Waziri wa Maliasili na Utalii.
Historia yake Lazaro Nyalandu
alizaliwa Agosti 18, 1970 mkoani Singida.
Nyalandu alipata elimu ya
msingi katika shule za Pohama na Mrumba zilizoko kijijini kwao huko mkoani
Singida na kuhitimu mwaka 1987.
Aliendelea na masomo ya kidato
cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Kibaha mkoani Pwani (1988 –1991)
na alifaulu vizuri na kujiunga na Shule ya Sekondari Ilboru ambako alisoma
kidato cha tano na sita.
Wakati akiwa mwanafunzi wa sekondari,Nyalandu alikuwa kiongozi wa juu wa Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania(Ukwata) 1991–1993 na baadaye alikuwa miongoni mwa vijana wa Kitanzania walioteuliwa kuzuru jiji la Rio De Janeiro,Brazil na kushuhudia mkutano wa Mazingira mwaka 1993.

Nyalandu alipata elimu yake ya
Chuo Kikuu nchini Marekani ambako alihitimu Shahada ya kwanza ya Sanaa katika
Usimamizi wa Biashara (BBA) mwaka 1997 katika Chuo Kikuu cha Wartburg.
Kabla ya hapo alikuwa amepata
Shahada ya Biashara ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Wardorf nchini humo.
Kiongozi huyu, ana Shahada ya Uzamili aliyoipata kwa njia ya utafiti kutoka
Chuo Kikuu cha Buckingham, Uingereza akifuzu katika masuala ya Ushirikiano wa
Kimataifa na Diplomasia.
Baada ya kuhitimu masomo yake
ughaibuni,Nyalandu alianza kazi huko huko Marekani katika Benki ya North West,akifanya
kazi katika kitengo cha operesheni za kibenki kati ya mwaka 1998–1999.
Aliporejea nchini Tanzania
alifanikiwa kuwa sehemu ya washauri wa mke wa aliyekuwa Rais Benjamin Mkapa,
Mama Anna Mkapa, katika uendeshaji wa taasisi ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote
(EOTF).
Ushauri wa timu yake ulisaidia
taasisi hiyo kupata misaada mingi kutoka nchi za Ulaya,Marekani,China na
nyinginezo.
Pia,alikuwa anamsaidia mama
huyo katika uandishi wa hotuba zake pale alipokuwa na majukumu makubwa ya
kitaifa na kimataifa.
Nyalandu amemwoa mrembo wa
Tanzania mwaka 2004 ‘Miss Tanzania’,Faraja Kotta na wana watoto wawili,Sarah na
Christopher.
Mbio za ubunge
Tangu alipokuwa kijana mdogo,Nyalandu
alionyesha kila dalili kuwa na nyota ya uongozi.Watu wanaomfahamu hawakushangaa
walipomwona mwaka 2000 anaingia kwenye mpambano ndani ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) akilisaka jimbo la Singida Kaskazini.
Kutokana na udhaifu wa upinzani
uliokuwepo wakati huo alijua atakuwa na kazi kubwa ndani ya chama chake tu,
hivyo,alipopitishwa na CCM akapambana majukwaani na wapinzani na kuwa mbunge.
Mwaka 2005,Nyalandu alipitishwa
tena na chama chake kuwania ubunge Singida Kaskazini,akakutana tena na upinzani
dhaifu kutoka kwa Kimia Omari Rashid wa Chadema,akajivunia asilimia 93.5 ya
kura zote na kuwa mbunge hadi mwaka 2010.
Baada ya kupata uzoefu wa
ubunge,kwa miaka kumi, Nyalandu alirudi tena kutetea mara ya tatu;CCM ikampa
nafasi mwaka 2010 na wananchi wakamchagua kwa ushindi wa asilimia 87.7
akimshinda kwa mara nyingine mgombea yuleyule wa Chadema wa mwaka 2005.
Ushindi wa mara hii ulikuja na bahati kubwa kwa Nyalandu.Bahati ya kwanza ilikuwa kukwea ngazi zaidi. Rais Jakaya Kikwete alimteua Nyalandu kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Novemba 2010 na alidumu hapo hadi Mei 2011 alipohamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii,nafasi aliyokaa kwa takriban miaka mitatu.
Bahati ya pili,Januari 2014,nyota yake ilipaa zaidi akapewa wadhifa mkubwa;mara hii akiteuliwa kuwa waziri kamili wa Maliasili na Utalii,sekta ambayo ina changamoto kubwa sana hapa nchini.

Mbio za urais
Nyalandu aliweka wazi nia yake
ya kuwania urais Desemba 28,2014 na alitangaza nia hiyo ya kugombea urais
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Ilongero,katika jimbo
analoliongoza,Singida Kaskazini, wakati akihutubia mamia ya wananchi.
Katika mkutano huo alisisitiza
kuwa“sasa ni zamu ya vijana kuongoza nchi”huku akiwaambia wananchi kuwa safari
yake ya ubunge kwa miaka 15 inaanzisha safari nyingine bila kuwaeleza ikiwa
bado ana nia na ubunge au la.
Aliambatana na mkewe,watoto
wake pamoja na wazazi wake.
Kabla ya kutangaza nia ya urais,Nyalandu aliwahi kusikika akisema kuwa “…siwezi kutangaza kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao bila kutumwa na watu” lakini kabla watu wenyewe hawajamtuma aliibuka na kuwaita yeye mwenyewe mkutanoni na kuweka nia yake.

Nguvu yake Nyalandu ni msomi
mwenye jitihada kubwa. Si mwanasiasa mzembe au aliyekimbia umande; aliusaka
kokote kule na leo hii anaweza kuingia kwenye mizani ya kupimwa kama mtu
anayeweza kuongoza nchi au la. Nyalandu ana shahada tatu za chuo kikuu.
Tukumbuke kuwa amekuwa mtu wa
karibu na mama Anna Mkapa kwa kipindi kirefu na mwanya huo aliutumia pia kuwa
na mawasiliano na Rais Mkapa na hata alipokuwa mbunge akazidi kujijenga.
Baadhi ya makada muhimu ndani
ya CCM wanamtaja vizuri na hii ni nafuu kubwa kwa mwanasiasa anayesaka kuingia
Ikulu.
Pia,ana uzoefu wa kukaa bungeni
kwa miaka 15.Huu ni uzoefu wa kipekee kabisa.Alipoingia bungeni,kwa mara ya
kwanza,alikuwa kijana wa miaka 30 leo ana miaka 47. Utumishi wa chombo kikubwa
kama Bunge kwa miaka 17 ni turufu muhimu sana kwake na inamwongezea sifa muhimu
za kumbeba katika kinyang’anyiro.
Udhaifu wake
Pamoja na kutangaza nia ya kuwania
urais,Nyalandu bado hajatangazika sana
Comments