UHURU KENYATA NA URAIS MWAKA 2017
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi
IEBC Wafula Chebukati amesema kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia
uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa na asilimia 0.96.
Bw
Chebukati amesema jumla ya wapiga kura 7,616,217 kati ya jumla ya wapiga kura
19.6 milioni ambao wamejiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo walishiriki
uchaguzi huo wa Alhamisi wiki iliyopita.
Hiyo ni asilimia 38.84.
Rais Kenyatta, akihutubu baada ya
kutangazwa mshindi, amewashukuru waliompigia kura.
Amesema uchaguzi uliomalizika ni
ishara ya uthabiti wa demokrasia na uthabiti wa taasisi za Kenya pamoja na
Wakenya wenyewe.
"Agosti 8, na sitachoka,
Wakenya walirauka kupiga kura. Na siku hiyo walinichagua bila shaka. Ushindi
wangu ulipopingwa Mahakama ya Juu, kwenye hukumu, mahakama haikupinga ushindi
wangu wa 54%. Takwimu hazikupingwa. Kilichokosolewa ni utaratibu uliopelekea
ushindi wangu," amesema.
Bw Odinga alikuwa ametarajiwa
kutangaza mwelekeo kwa wafuasi wake baada ya tangazo la matokeo kufanywa na Bw
Chebukati.
Taarifa zinasema ameamua kufanya
hivyo hapo kesho.
Matokeo kamili ya wagombea wote kama yalivyotangazwa na Bw
Chebukati
Mgombea
|
Chama
|
Kura
|
Asilimia
|
Uhuru
Kenyatta
|
Jubilee
|
7,483,895
|
98.28
|
Raila
Odinga (Alisusia)
|
ODM
|
73,228
|
0.96
|
Mohamed
Abduba Dida
|
ARK
|
14,107
|
0.19
|
Japheth
Kavinga Kaluyu
|
Mgombea
wa kujitegemea
|
8,261
|
0.11
|
Michael
Wainaina Mwaura
|
Mgombea
wa kujitegemea
|
6,007
|
0.08
|
Joseph
Nthiga Nyagah
|
Mgombea
wa kujitegemea
|
5,554
|
0.07
|
John
Ekuru Aukot
|
Thirdway
Alliance
|
21,333
|
0.28
|
Cyrus
Jirongo
|
UDP
|
3,832
|
0.05
|
Bw Chebukati amesema anaamini
uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.
Mwenyekiti huyo amesema mambo
aliyosema yalihitajika kufanyika kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki
yalitimizwa.
Amesema walitaka kuhakikisha kila
kitu kilikuwa sawa.
"Hata tulibadilisha tarehe
kutoka 17 hadi 26 Oktoba kuhakikisha tuna muda wa kutosha," amesema.
Kadhalika, amesema alikuwa na
kundi la kusimamia mradi wa uchaguzi wa urais kuondoa majukumu kutoka kwa
makamishna ambao walituhumiwa na baadhi ya wadau.
"Naweza kusema kwa uhakika,
kwamba 26 Oktoba kabla ya uchaguzi kuanza, nilikuwa nimeridhika kwamba tulikuwa
tumefanya kila kitu kuhakikisha kila Mkenya angetekeleza haki yake
kikatiba," amesema.
"Na haki hii mtu anafaa
kuitekeleza bila kutishiwa au kuzuiwa."
Bw Chebukati anasema alishangaa
kwamba watu waliotafuta wa kushambulia walimwendea yeye.
Hata hivyo, anasema ndani ya tume
nao walimwogopa.
"Hatutaweza kufurahisa kila
mtu. Nimedumisha na kuheshimu sheria, kama mwanasheria ziwezi kuvunja sheria
niliyojitolea kuilinda," amesema.
Matokeo yalivyokuwa uchaguzi wa
tarehe 8 Agosti ambao ulifutwa na Mahakama ya Juu
Mgombea
|
Chama
|
Kura
|
Asilimia
|
Uhuru
Kenyatta
|
Jubilee
|
8,203,290
|
54.27
|
Raila
Odinga
|
ODM
|
6,762,224
|
44.74
|
Mohamed
Abduba Dida
|
ARK
|
38,093
|
0.25
|
Japheth
Kavinga Kaluyu
|
Mgombea
wa kujitegemea
|
16,482
|
0.08
|
Michael
Wainaina Mwaura
|
Mgombea
wa kujitegemea
|
13,257
|
0.09
|
Joseph
Nthiga Nyagah
|
Mgombea
wa kujitegemea
|
42,259
|
0.28
|
John
Ekuru Aukot
|
Thirdway
Alliance
|
27,311
|
0.18
|
Cyrus
Jirongo
|
UDP
|
11,705
|
0.08
|
Comments