SERIKALI KUFUNGUA UTALII KANDA YA KUSINI
Na.Issack Gerald-Rukwa
Serikali imesema imedhamiria kufungua utalii
wa Kanda ya Kusini ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini na hatimaye
kuongeza idadi ya watalii na kipato kwa Serikali na jamii kwa ujumla.
Hatua hiyo imeelezwa na Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga katika kijiji cha Kapozwa Wilayani Kalambo
Mkoani Rukwa,wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea Maporomoko ya Mto
Kalambo ambayo ni ya pili kwa kina kirefu barani Afrika.
Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali wa maendeleo ikiwemo benki ya Dunia kupitia mradi wa REGROW imepanga
kuboresha miundombinu ya vivutio vya utalii vya Kanda ya Kusini na kuvitangaza,ili
kuimarisha sekta hiyo muhimu ambayo inachangia asilimia 25 ya mapato yote ya
kigeni na asilimia 17.5 ya pato la taifa.
Aidha,ametoa wito kwa wananchi wa kijiji cha
Kapozwa wanaoishi jirani na hifadhi kushirikiana na Serikali katika uhifadhi wa
uoto wa asili pamoja na kudumisha tamaduni zao.
Vivutio vingine ni pamoja na Hifadhi ya Taifa
ya Katavi ambayo ni ya tatu kwa ukubwa nchini,Hifadhi ya Taifa ya
Udzungwa,Mikumi,Mahale,Gombe,Pori la Akiba la Selous, Hifadhi ya Mazingira
Asilia ya Mlima Rugwe na Kimondo cha Mbozi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments