Posts

Showing posts from November 9, 2017

CHANZO CHA BOMU KUUA WANAFUNZI 9 MKOANI KAGERA HIKI HAPA

Image
Na.Issack Gerald Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Kagera Agustino Olomi amesema chanzo cha wanafunzi kupoteza maisha na kujeruhiwa kwa bomu ni kutokana na Mwanafunzi kuokota bomu hilo akidhani chuma chakavu ili akauze. Katika taarifa aliyoitoa akizungumza na Wanahabari Kamanda Olomi amesema,katika kijiji hicho kumekuwa na tabia ya kuuza vyuma chakavu ambapo mnunuzi huwa akiwapatia malipo ya madaftari. Kwa upande wa Kamanda wa Kikosi cha kulinda mipaka cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wilayani Ngara Meja TR Mutaguzwa amesema,Bomu hilo lilikuwa na vipande 36 na lingelipukia ndani ya darasa lingeleta athari zaidi . Jumla ya wanafunzi 9 walifariki dunia na wengine 25 kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu hilo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAZIRI WA ELIMU AMETOA AGIZO KALI KWA WAKUU WA VYUO ELIMU YA JUU

Image
Na.Issack Gerald Serikali imewaagiza wakuu wote wa vyuo vya elimu ya juu kuacha urasimu katika utoaji wa fedha kwa wanufaika wa mikopo ambao wana makubaliano na Serikali. Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema leo bungeni ikiwa ni utekelezaji  wa agizo la Spika Job Ndugai  lililotaka serikali kutoa kauli kuhusu wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutakiwa kutoa fedha ili wasajiliwe kabla ya kupata  mikopo. Agizo la Spika lilitokana na Mwongozo uliombwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Martha Mlata ambaye alieleza bunge kuwa wanafunzi wamekuwa wakihangaika vyuoni baada ya kutakiwa walipe fedha za usajili kabla ya kupewa mkopo. Amesema inasikitisha sana kuona baadhi ya vyuo vinadiriki hata kuwakataa wanafunzi waliowadahili wao wenyewe au vinawalazimisha wachukue programu tofauti na walizokuwa wamechaguliwa awali na vyuo husika. Amesema Serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa vyuo vyote vitakavyoleta usumbufu usio wa lazima kwa wanaf...

VYOMBO VYA DOLA VIPEWE MUDA WA KUCHUNGUZA MATUKIO YA MAUAJI

Image
Na.Issack Gerald Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema vyombo vya dola vinatakiwa kupewa muda kwa ajili ya kufanya uchunguzi katika matukio mbalimbali ya mashambulizi dhidi ya wananchi na viongozi. Waziri Mkuu amesema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma, wakati wa maswali na majibu mara baada ya kuulizwa swali na kiongozi wa kambi rasmi bungeni,Freeman Mbowe kuhusu kurusu vyombo vya kimataifa kufanya uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu Aidha ameongeza kuwa Tundu Lissu ni mbunge mwenzao hivyo suala hilo linamhusu kila mbunge wa kutoka upande wowote,hivyo linashughulikiwa kama matukio mengine yanavyoshughulikiwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS AMEMTUMBUA MKURUGENZI MTENDAJI MWINGINE

Image
Na.Issack Gerald Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw.Abdallah Hussein Mussa kwa kushindwa kumudu majukumu yake. Katibu mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe ametoa taarifa hiyo ya kutenguliwa kwa mkurugenzi huyo leo mjini Dodoma. Kwa mjibu wa Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini Rebecca Kwandu,uteuzi wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru utafanywa baadaye. Wiki iliyopita Rais Magufuli alitengua nafasi ya wakurugenzi wa tendaji wawili wa Manispaa ya Bukoba na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAZIRI MKUU:KATIBA SIYO KIPAUMBELE CHA SERIKALI KWA SASA

Image
Na.Issack Gerald Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Changamoto za jamii ni nyingi kuliko mahitaji ya Katiba hivyo suala la katiba sio kipaumbele cha serikali kwa sasa. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Bungeni wakati wa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu,ambapo alijibu swali la Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea lililohoji kuwa ‘Serikali ya awamu ya tano imetimiza miaka miwili lakini hakuna jitihada zozote zilizofanywa katika kuendeleza mchakato wa katiba ulioachwa na Serikali ya awamu ya nne. Waziri Majaliwa ameongeza kuwa Katiba ni muongozo tu na wakati ukifika serikali yake imemaliza changamoto basi wataanza mchakato huo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED