AMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUBAKA MWANAFUNZI
Na.Issack Gerald-Katavi
Mahakama
ya wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imemuhukumu
kifungo cha maisha Lazaro Ngomalala(50)mkazi wa Kijiji cha
Sibwesa wilayani Tanganyika baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka
mwanafunzi wa darasa la pili(9)wa shule ya msingi Sibwesa.
Akisoma
hukumu hiyo juzi,hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mpanda Chiganga
Tengwa alisema mahakama imeridhika na ushahidi
wa mashahidi sita wa upande wa mashitaka uliotolewa
mahakamani hapo ukiwemo wa mwanafunzi aliyebakwa.
Kabla
ya kutoa hukumu hiyo Hakimu Tengwa alisema mtu
yoyote anayefanya kitendo kama alichofanyiwa mtoto
huyo anakuwa amefanya kosa kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba
130(1)na(2) na kifungu cha sheria namba 131(3) cha kanuni
ya adhabu.
Hakimu
Tengwa alisema miongoni mwa ushahidi uliosababisha
mahakama imtie hatiani mtuhumiwa ni ushahidi uliotolewa
na mtoto aliyebakwa pamoja na mtoto mwenzake mwenye umri wa miaka
saba licha ya kuwa na umri mdogo walitoa
ushahidi kwa ufasaha mkubwa dhidi ya tukio hilo.
Pia Mahakama ilijiridhisha
na ushahidi uliotolewa na muuguzi wa
Zahanati ya Sibwesa aliyeamchunguza na kubaini kuwa kubaini mtoto huyo alikuwa amembakwa alimwanzishia dawa
ya kuzuia maambukizi ya virus vya ukimwi.
Katika
kujitetea mtuhumiwa ,aliiomba Mahakama kumwachia huru akidai
yeye hakutenda kos hilo bali alisingiziwa
na mama mzazi wa mtoto huyo kwa kuwa alikuwa
akimdai fedha alizomkopesha.
Baada
ya utetezi huo hakimu Tengwa alisema kutokana na mshitakiwa kupatika na hatia
Chini ya kifungu cha sheria namba131(3),mtu
yoyote atakae mbaka mtoto mwenye umri wa miaka chini ya (10) adhabu
yake ni kifungo cha maisha jela.
Hivyo
kutokana na mshitakiwa
Ngomalala kupatikana na kosa hilo
mahakama imemuhukumu kuanzia jana kutumkia kifungo
cha maisha jela.
Awali kwenye kesi hiyo
Wakili
wa Serikali Fravian Shiyo alidai Mahakamani hapo
kuwa Lazaro alitenda kosa hilo
Oktoba 12 mwaka jana majira ya saa
4 asubuhi kijijini hapo.
Ilidaiwa
kuwa siku
ya tukio mshitakiwa alikuta mtoto
aliyemtendea kitendo hicho akiwa
na mtoto mwenzake wakiwa wanacheza jirani na nyumba
yao ndipo alipowadanganya wafuate nyumbani
kwake ili akawape fedha wakanunue biscuit na soda.
Mwanasheria
aliiambia mahakama hiyo baada ya kufanyiwa kitendo hicho
mtoto huyo aliyebakwa alikwenda kutoa taarifa
kwa wazazi wake huku akiwa analia na wazazi wake
walitoa taarifa kwa askari mgambo wa kijiji ambaye
alimkamata na kumfikisha kituo cha polisi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments