RAIS AMEMTUMBUA MKURUGENZI MTENDAJI MWINGINE
Na.Issack Gerald
Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi
wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw.Abdallah Hussein Mussa kwa
kushindwa kumudu majukumu yake.
Katibu
mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Mhandisi
Mussa Iyombe ametoa taarifa hiyo ya kutenguliwa kwa mkurugenzi huyo leo mjini
Dodoma.
Kwa
mjibu wa Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini Rebecca Kwandu,uteuzi wa
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru utafanywa baadaye.
Wiki
iliyopita Rais Magufuli alitengua nafasi ya wakurugenzi wa tendaji wawili wa
Manispaa ya Bukoba na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments