WAKAZI HALMASHAURI YA NSIMBO WALILIA BARABARA



Na.Issack Gerald-Katavi
Wakazi wa kata ya Itenka iliyopo halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wameiomba serikali kuwatengezea barabara ya Imilamate-Itenka hadi mjini Mpanda.
Kwa mujibu wa baadhi ya wakazi wa kata hiyo,wamesema licha ya barabara hiyo kuwa kitovu cha mawasiliano lakini imetelekezwa na serikali.
Wamsema wanahofia uhakika wa barabara hiyo kupitika hasa katika musimu huu wa mvua kwani imekuwa ikikatika na wao kubaki wako kisiwani.
Akijibu hoja za wananchi hao,mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Raphael Kalinga amesema tayari halmashauri imeshawasilisha makadirio ya barabara zote kwa wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) wanachosubiri ni utekelezaji
Bwana Kalinga amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati huu ambapo bado barabara hiyo ipo kwenye mchakato wa matengenezo.
Mwaka 2016 barabara kutoka Kitongoji cha Tumaini-Imilamate-Itenka ilikuwa imewekewa changalawe na hivyo kupitika kwa muda tofauti na hali ilivyokuwa.
Kata hiyo ni moja kati ya vyanzo vya mapato vya Halmshauri kutokna na kuendeshwa kwa kilimo hasa zao la Mpunga.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA