CHANZO CHA BOMU KUUA WANAFUNZI 9 MKOANI KAGERA HIKI HAPA
Na.Issack Gerald
Kamanda
wa jeshi la polisi Mkoani Kagera Agustino Olomi amesema chanzo cha wanafunzi
kupoteza maisha na kujeruhiwa kwa bomu ni kutokana na Mwanafunzi kuokota bomu
hilo akidhani chuma chakavu ili akauze.
Katika taarifa aliyoitoa akizungumza na Wanahabari Kamanda
Olomi amesema,katika kijiji hicho kumekuwa na tabia ya kuuza vyuma chakavu
ambapo mnunuzi huwa akiwapatia malipo ya madaftari.
Kwa upande wa Kamanda wa Kikosi cha kulinda mipaka cha Jeshi
la Wananchi wa Tanzania JWTZ wilayani Ngara Meja TR Mutaguzwa amesema,Bomu hilo
lilikuwa na vipande 36 na lingelipukia ndani ya darasa lingeleta athari zaidi .
Jumla ya wanafunzi 9 walifariki dunia na wengine 25 kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu hilo.
Jumla ya wanafunzi 9 walifariki dunia na wengine 25 kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu hilo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments