UHURU KENYATA NA URAIS MWAKA 2017
Rais Uhuru Kenyatta ametangazwa mshindi wa urais wa marudio nchini Kenya akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98%. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati amesema kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa na asilimia 0.96. Bw Chebukati amesema jumla ya wapiga kura 7,616,217 kati ya jumla ya wapiga kura 19.6 milioni ambao wamejiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo walishiriki uchaguzi huo wa Alhamisi wiki iliyopita. Hiyo ni asilimia 38.84. Rais Kenyatta, akihutubu baada ya kutangazwa mshindi, amewashukuru waliompigia kura. Amesema uchaguzi uliomalizika ni ishara ya uthabiti wa demokrasia na uthabiti wa taasisi za Kenya pamoja na Wakenya wenyewe. "Agosti 8, na sitachoka, Wakenya walirauka kupiga kura. Na siku hiyo walinichagua bila shaka. Ushindi wangu ulipopingwa Mahakama ya Juu, kwenye hukumu, mahakama haikupinga ushindi wangu wa 54%. Takwimu hazikupingwa. Kilichokosolewa ni utaratibu uliopelekea ushindi wangu,...