ASILIMIA 90 YA WACHIMBAJI MADINI MKOANI KATAVI WANACHIMBA MADINI BILA UTAFITI
Na.Issack Gerald-Katavi Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Magharibi Mhandisi Juma Haruna Sementa,amesema asilimia 90 ya wachimbaji wa madini Mkoani Katavi,wanashindwa kufikia malengo katika uchimbaji madini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutofanya utafiti kabla ya kuchimba. Mhandisi Sementa amesema hayo wakati akizungumzia kuhusu baadhi maeneo ya uchimbaji kutelekezwa ikiwemo maeneo ya Kapalamsenga. Ametaja sababu nyingine inayokwamisha uchimbaji endelevu wa madini mkoani Katavi kuwa ni ukosefu wa mtaji wa fedha za kuendeshea mitambo. Katika hatua nyingine Kamishna Sementa amesema ujenzi wa kituo cha mfano cha kuchenjua madini kilichokuwa kimepangwa kukamilika ujenzi wake mwezi Septemba mwaka huu katika machimbo ya Kapanda,bado haujatekelezwa kutokana na uhaba wa fedha. Hata hivyo ametaja shughuli za uchimbaji madini bila utafiti ndiyo chanzo kinachopelekea uharibifu wa mazingira. Baadhi ya maeneo yanayotajwa kuwa na madini hususani dhahabu Mkoani Katavi ni pamo...