MIKOA 11 YATAHADHARISHWA NA TMA KUHUSU MVUA KUBWA
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),imetoa tahadhari ya vipindi vya mvua kubwa vinavyotarajiwa kuendelea katika maeneo ya mikoa 11 nchini. TMA imetaja mikoa itakayoathirika na mvua hizo ni Dar es Salaam,Pwani,Lindi,Mtwara,Morogoro,Ruvuma,Rukwa, Mbeya,Songwe,Iringa na Njombe. Taarifa iliyotolewa leo na mamlaka hiyo inabainisha kuwa kuanzia leo Machi 12 hadi 13,2018 kunatarajiwa vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24. Taarifa hiyo inaeleza kuwa hali hiyo inatokana na kuendelea kuimarika kwa ukanda wa mvua huku wakazi wa maeneo yaliyotajwa wakitakiwa kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa na tahadhari zinazotolewa. Aidha TMA imesema inaendelea kufuatilia hali hiyo na itatoa mrejesho kila itakapobidi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED