MIKOA 11 YATAHADHARISHWA NA TMA KUHUSU MVUA KUBWA
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),imetoa tahadhari ya vipindi vya mvua kubwa
vinavyotarajiwa kuendelea katika maeneo ya mikoa 11 nchini.
TMA
imetaja mikoa itakayoathirika na mvua hizo ni Dar es Salaam,Pwani,Lindi,Mtwara,Morogoro,Ruvuma,Rukwa,
Mbeya,Songwe,Iringa na Njombe.
Taarifa
iliyotolewa leo na mamlaka hiyo inabainisha kuwa kuanzia leo Machi 12 hadi 13,2018
kunatarajiwa vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24.
Taarifa
hiyo inaeleza kuwa hali hiyo inatokana na kuendelea kuimarika kwa ukanda wa
mvua huku wakazi wa maeneo yaliyotajwa wakitakiwa kuchukua tahadhari stahiki na
kuendelea kufuatilia taarifa na tahadhari zinazotolewa.
Aidha
TMA imesema inaendelea kufuatilia hali hiyo na itatoa mrejesho kila itakapobidi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments