FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM
Jokate Mwegelo
|
|
Amezaliwa
|
|
Utaifa
|
|
Kazi yake
|
Mwigizaji, mjasiriamali, mtangazaji, mwimbaji
|
Miaka ya kazi
|
2006-hadi sasa
|
Jokate Mwegelo ni mwigizaji wa filamu na mjasiriamali kutoka nchini Tanzania. Jokate vilevile ni mtangazaji na mwimbaji.
Huyu ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Kidoti Company.Mwaka wa
2011,alishinda tuzo ya Zanzibar International Film Festival akiwa kama
mwigizaji bora filamu wa kike.Mwaka wa 2017,Mwegelo aliingizwa katika jarida la
Forbes katika Forbes 30
Under 30 kutoka Afrika.
MAISHA YA AWALI NA ELIMU.
Mwegelo alizaliwa
mnamo tarehe 20 Machi,1987 huko mjini Washington
D.C ambapo wakati huo wazazi wake
walikuwa wanafanya kazi.Alikulia jijini Dar
es Salaam, Tanzania.Alianza elimu ya msingi katika shule ya Olympio
Primary School na baadaye St.Anthony High School, halafu Loyola High School,Dar
Es Salaam,Tanzania. Alihitimu katika Chuo Kikuu cha
Dar Es Salaam ambapo alipata shahada ya sayansi ya siasa na falsafa.
MISS TANZANIA 2006
Alikuwa
mshindi wa pili katika shinda la Miss
Tanzania mwaka 2006.Vilevile alipewa jina la balozi wa Redds
fashion na balozi wa gazeti la Citizen,baada ya kupata kura nyingi mwaka huo.Kabla
ya Miss Tanzania, alishindana katika Miss Kurasini 2006,shindano ambalo
alishinda kisha kuelekea juu zaidi na kuwa Miss Temeke 2006 ambako pia alishinda.
KAZI
Kuigiza
Mwaka wa 2007,alipata
kucheza filamu yake ya kwanza iliyojulikana kwa jina la Fake Pastors,akiwa na Vincent Kigosi,Lisa Jensen,mshindi wa tatu wa Miss Tanzania
2006 na marehemu Adam Kuambiana.Mwaka
wa 2008, amecheza katika filamu ya From
China With True Love.Mwaka wa 2010,alionekana katika filamu ya Chumo,filamu
iliyoandaliwa na Media for Development International, kuhusu
elimu juu ya ugonjwa wa malaria. Filamu hii
ilimwezesha kupata tuzo ya Zanzibar International Film Festival akiwa
kama mwigizaji bora wa kike kwa 2011 na kuchaguliwa kama mwigizaji wa
Pan-Afrika katika tuzo za 2012
Nigeria Entertainment Awards. Vilevile amepata kuonekana katika mfululizo
wa TV maarufu wa Siri Ya
Mtungi,uliokuwa unaandaliwa na Jordan Riber na kuongozwa na Karabani,
mnamo 2013.Mwaka wa 2014, amecheza uhusika wa "Ndekwa" katika filamu
ya Mikono Salama,ambayo ilimpelekea apate tuzo nyingine ya Zanzibar International Film Festival akiwa
mwigizaji bora wa kike kwa filamu za Kiswahili.
Kampuni ya Kidoti
Muziki
Alishirikishwa
katika wimbo wa Japo Nafasi wa Cpwaa akiwa
na A.Y. katika
wimbo wa Kings and Queen na Amani,kutoka Kenya.Mwaaka
wa 2013, alitoa wimbo wake akiwa na Lucci,uliyoitwa
'Kaka na Dada.Mwaka wa 2015 akadondosha wimbo wake mwingine uliyoitwa
Leo akiwa na mwimbaji mwingine kutoka nchini Nigeria maarufu kama Ice Prince.
Miezi 11 iliyopitia aliteuliwa na UVCCM kuwa Kaimu
Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM Taifa.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments