MAASKOFU WAANZA KUTEMA CHECHE SUALA LA KATIBA MPYA NA USALAMA WA TAIFA
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dk.Fredrick
Shoo amesema kama taifa linahitaji maendeleo ya kweli basi kuna haja ya kuwa na
katiba mpya na si iliyopo sasa.
Askofu Dk.Fredrick Shoo |
Askofu Dk Fredrick Shoo alisema hayo baada ya kutoa ujumbe wa
Pasaka na kusema kuna haja ya kuwa na katiba mpya ili kuweza kupata maendeleo
ya kweli kwani katiba mpya ndiyo inaweza kuongoza kila raia.
"Katiba iongoze kila raia, utaratibu wa Watanzania kuweza
kuishi pamoja na kama tunataka maendeleo ya kweli pasipo Katiba mpya tutakuwa
tunajidanganya" alisema Askofu
Shoo
Mbali na hilo
Askofu Shoo aliweza kuzungumzia mambo mengi kuhusu usalama wa nchi na watu wake
na kuonyesha wasiwasi kuwa kuna vitu haviendi sawa kutokana na kuibuka kwa
mambo ambayo si utamaduni wa Tanzania, kama watu kupigwa risasi, kuokotwa kwa
miili ya watu baharini, kuuwawa kwa watu katika mazingira ya kutatanisha.
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments