UYOGA WAUA WAWILI KATAVI NA WENGINE MAHUTUTI
Watu wawili ambao wametambulika kwa majina Frenki
Mayaga na Erizabeth George wakazi wa kijiji cha Stalike wilayani Mpanda mkoani Katavi,wafamefariki
dunia baada ya kula uyoga unaotajwa kuwa na Sumu.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Christopher Anjero amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo leo ambapo amesema mbali na marehemu hao,watu wengine watatu wako mahututi na
wanaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mpanda.
Bi.Monica George ambaye ni miongoni mwa ndugu
wa marehemu amesema walikwenda porini kutafuta uyoga ambapo baada ya kupika na kula
ndiyo wakapatwa na mauti hayo.
Aidha George Anjero Mrisho amesema alipokea
taarifa za kifo cha kijana wake Frenki Mayaga akiwa shambani.
Hata hivyo Mganga wa zamu wa hospitali ya
Manispaa ya Mpanda hakuupatikana ili kujua taratibu za kitabibu zinazoendelea kwa
sababu hakuwepo kituoni.
Kwa mjibu wa mwenyekiti wa kijiji cha Sitalike
Bw. Christopher
Anjero hilo ni tukio la kwanza katika kipindi cha miaka 10 iliyopita
ndani ya uongozi wake.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments