MGOMO DARADARA MPANDA NAULI KUPUNGUZWA,SUMATRA YASEMA WASIOTAKA NAULI ILIYOPANGWA NA SUMATRA WAPAKI MAGARI
Baadhi ya daradara mjini Mpanda zikiwa zimepaki baada ya madereva kusitisha safari Na.Issack Gerald-Katavi Madereva wa daradara zinazosafirisha abiria kutoka Mpanda Mjini kuelekea kata ya Kakese leo wamegoma na kumlalamikia Meneja wa mamlaka ya uasafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi kwa kushusha viwango vya nauli.