KIONGOZI MBIO ZA MWENGE MPANDA - ACHENI KUTOA NA KUPOKEA RUSHWA KUPATA VIONGOZI BORA
Na.Issack
Gerald-Katavi
JAMII
mkoani Katavi imetakiwa kuwafichua wagombea wanaotoa rushwa kupata uongozi
katika uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwaka huu, ili wapatikane viongozi
bora watakaojali maslahi yao.
Wito
huo umetolewa jana na Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Bw. Juma Khatib Chum katika shule ya
sekondari ya kasimba wakati akizindua miradi ya maendeleo.
Muiongoni
mwa miradi iliyozinduliwa jana ni pamoja na klabu ya kupinga madawa ya kulevya
katika shule ya sekondari Kasimba, wodi ya akina mama kituo cha afya Mwangaza,
ofisi ya mtendaji wa kata ya Makanyagio, klabu ya kuzuia maambukizi ya Ukimwi
shule ya msingi Katavi.
Mwenge
wa uhuru umewasili jana Halmshauri ya Mji wa Mpanda ukitokea Wilayani Nkasi Mkoani
Rukwa ambapo leo umeendelea na safari zake katika Halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda na kesho utaelekea Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo na kuhitimisha mbio
zake Halmsjhauri ya Wilaya ya Mlele na hatimaye kupokelewa Mkoani Tabora.
Kauli
mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka huu ni “Tumia haki yako kidemokrasia jiandikishe
na upige kura katika uchaguzi wa 2015.”
Comments