WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMTUPA TAKUKURU MKURUGENZI MUWASA.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa ameamuru Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoani Mara kumkamata na kumuhoji Mkurugenzi Mtendani wa Mamlaka ya Maji Musoma (Muwasa) Gantala Said kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mradi wa maji Bunda. Mbali na mkurugenzi huyo pia ameiagiza Takukuru imuhoji mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Nyakirang'anyi,Mahuza Mumay ambaye ndiye mkandarasi anajenga mradi huo unaotoa maji kutoka Ziwa Victoria katika eneo la Nyabehu hadi Bunda mjini. Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo jana baada ya mkurugenzi huyo kushindwa kueleza kitu kilichosababisha mradi wa maji Bunda kutokamilika pamoja na Serikali kutoa fedha nyingi. Akizungumza katika kikao maalumu cha kujadili changamoto za utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Mara, alichokiitisha mjini Bunda, Waziri Mkuu alisema alimua kuitisha kikao hicho baada ya kutoridhishwa na utekelezwaji wa miradi hiyo hususan inayosimamiwa na Muwasa. Alisema kwa sasa Serikali inatekeleza kampeni ya Rais John ...