SERIKALI YAKATAZA KULIMA PAMBA KWA MKATABA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
Serikali imekataza kilimo cha pamba cha mkataba kwa sababu kinawanyonya
wakulima.
Ameyasema hayo jana (Ijumaa, Januari
19, 2018) wakati akizungumza na wananchi baada ya kukagua zahanati ya Hunyari
wilayani Bunda, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mara.
Alisema Serikali imeweka mkakati wa
kuimarisha mazao makuu ya biashara ambayo uzalishaji wake umeanza kupungua
likiwemo na zao la pamba.
Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua
kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa kilimo cha zao la pamba kuanzia hatua
za maandalizi ya shamba,pembejeo hadi masoko.
Pia Waziri Mkuu amewaagiza Maofisa
Kilimo katika wilaya hiyo wawafuate wakulima vijijini kwa ajili ya kutoa elimu
itakayowawezesha wakulima kulima kwa kufuata njia bora za kisasa.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu
amewataka wafugaji kuhakikisha wanakuwa na idadi ya mifugo kulingana na uwezo
wa eneo lao.“Marufuku kulisha mifugo katika mashamba ya watu.”
Amesema Serikali itachukua hatua kali
za kisheria kwa mfugaji yeyote atakayelisha mifugo yake katika mashamba ya
wakulima kwani tabia hiyo huchangia migogo baina yao.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments