WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMTUPA TAKUKURU MKURUGENZI MUWASA.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa ameamuru
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoani Mara kumkamata na
kumuhoji Mkurugenzi Mtendani wa Mamlaka ya Maji Musoma (Muwasa) Gantala Said
kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mradi wa maji Bunda.
Mbali na mkurugenzi huyo pia
ameiagiza Takukuru imuhoji mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Nyakirang'anyi,Mahuza
Mumay ambaye ndiye mkandarasi anajenga mradi huo unaotoa maji kutoka Ziwa
Victoria katika eneo la Nyabehu hadi Bunda mjini.
Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo jana baada
ya mkurugenzi huyo kushindwa kueleza kitu kilichosababisha mradi wa maji Bunda
kutokamilika pamoja na Serikali kutoa
fedha nyingi.
Akizungumza katika kikao maalumu cha
kujadili changamoto za utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Mara,
alichokiitisha mjini Bunda, Waziri Mkuu alisema alimua kuitisha kikao hicho
baada ya kutoridhishwa na utekelezwaji wa miradi hiyo hususan inayosimamiwa na
Muwasa.
Alisema kwa sasa Serikali inatekeleza
kampeni ya Rais John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani. Kampeni hiyo inayolenga kuwaondolea wananchi tatizo la
upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama,hivyo itawachukulia hatua wote watakaokwamisha
miradi ya maji.
Waziri Mkuu alisema malengo ya
kampeni hiyo ni kuwafikishia wananchi huduma ya maji safi na salama katika
umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.
Wakati huo huo Majaliwa ameagiza
kupitiwa upya kwa mradi huo kwa sababu
hafurahishwi na ujenzi wake.
Alisema mkurugenzi huyo amekuwa
akimlipa mkandarasi fedha kabla ya kufanya kazi ambapo hadi sasa tayari
mkandarasi anayenga mradi huo ameshalipwa zaidi ya Sh 7 bilioni na mradi
haujakamilika na wananchi wanaendelea kutumia maji ambayo siyo salama.
Waziri Mkuu alisema viongozi hao
wahojiwe na wakibainika kuhusika na ubadhilifuu wa fedha za mradi huo,wachukuliwe
hatua kali za kisheria.
Mradi wa kupeleka maji kwenye mji wa
Bunda maji kutoka Ziwa Victoria katika eneo la Nyabeho ulisanifiwa mwaka 2006
na ulikuwa unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha za
maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara,
Adam Malima aliagiza kufungwa na ofisi za Muwasa na kuwataka wafanyakazi wa
mamlaka hiyo kutoruhusiwa kuingia ofisini hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments