WAZIRI MKUU ASEMA HANA KINYONGO NA MTU YEYOTE,ASEMA ITIKADI ZA SIASA ZILIISHIA OKTOBA 25
Na.OFISI YA WAZIRI MKUU. WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hana kinyongo na mtu yeyote kwa sababu alitangaza msamaha siku aliyokabidhiwa cheti kuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa na kusisitiza kuwa siasa ziliisha tangu Oktoba 25, mwaka huu. Waziri Mkuu Kasim Majaliwa akizungumza na Wakazi Mkoani Lindi