MAUAJI KATAVI
Na.Issack
Gerald- Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la KAZIMIRI MASUMBUKO(49) MKAZI NA MKULIMA WA
MISANGA aliuawa kwa kuchomwa kitu chenye ncha kali sehemu za mgongoni, mkononi,
mkono wa kushoto na kidevuni na watu wasiofahamika
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo,Kmanda
wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari,amesema tukio hilo limetokea jana
Jumapili tarehe 20.12.2015 majira ya saa katika kitongoji cha Misanga Kata na
Tarafa ya Mwese Wilayani Mpanda Mkoani Katavi. Kamanda wa polisi Katavi-Dhahiri Kidavashari |
Kamanda Kidavashari amesema kuwa, siku ya
tukio hilo,watuhumiwa wasiofahamika kwa sura wala idadi yao walifika nyumbani
kwa marehemu wakakuvunja mlango na kuingia moja kwa moja hadi chumbani kwa marehemu
na kumpeleka sebureni kwake kisha kutekeleza mauaji hayo na kutokomea
kusikojulikana .
Mpaka sasa chanzo cha tukio hilo bado
hakijafahamika. Hata hivyo Upelelezi wa shauri hili unaendelea kwa kufanya
msako kwa kushirikiana na wakazi wa kata ya Misanga kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa
na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili.
Wakati huo huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Katavi anatoa agizo kwa wananchi kuachana na vitendo vya kujichukulia sheria
mikononi dhidi ya migogoro ya kijamii miongoni mwao, badala yake wajenge tabia
ya kuheshimu na kutumia mamlaka za kisheria katika kutafuta ufumbuzi.
Amesisitiza kuwa ataendelea kuchukua hatua
kali za kisheria kwa wale watakaoendelea kubainika kukiuka maagizo hayo
kutokana na visingizio mbalimbali
Endelea
kufuatilia habari mbalimbali kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments