Posts

Showing posts from February 8, 2018

TANZANIA KUWA NA WATU 58 MILIONI IFIKAPO MWISHONI MWA 2018

Image
Tanzania inatarajiwa kufikisha idadi ya watu milioni 58 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la juu ikilinganishwa na idadi ya awali ya watu milioni 46 iliyoripotiwa mwaka 2010. Kwa mujibu wa Idara ya Jamii na Mambo ya Uchumi ya Shirika la Umoja wa Mataifa (UN),makadirio hayo ni sawa na kila kilomita moja ya mraba kuna wakazi 67 tofauti na makadirio ya mwaka 2010 ya watu 52. Inasema kila sekunde 14,mtoto mmoja anazaliwa nchini huku mtoto mmoja akifariki dunia kila baada ya sekunde moja.

KADA MKONGWE WA CHADEMA AFARIKI DUNIA

Image
Mwanasiasa mkongwe na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tambwe Hizza amefariki dunia asubuhi ya kuamkia leo (Alhamis ) akiwa nyumbani kwake kwa ugonjwa wa pumu. Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene amethibitisha kifo hicho akisema Hiza amefariki leo asubuhi nyumbani kwake Mbagala akiwa amelala. Hiza amefariki kipindi ambacho alikuwa katika timu ya kampeni za kumnadi mgombea wa ubunge wa Chama hicho katika Jimbo la Kinondoni, Salumu Mwalimu na jana jioni alipanda jukwaani kumnadi. Mwaka 2015,Hiza alitangaza kujiunga na Chadema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu akitokea CCM ambako aliwahi kuhudumu kama mkuu wa kitengo cha propaganda wa chama hicho tawala.

SERIKALI KUTATUA KERO YA MAJI VIJIJI VYA JIMBO LA KAVUU

Image
Wizara ya maliasili na utalii inatarajia kutatua kero ya maji kwa wakazi wa kata ya Itobanilo na vijiji vyake katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi,ili kuondoa mgogoro kati ya askari wa wanayama pori na wananchi wanaotegemea maji ya mto Kavuu uliopo hifadhi ya taifa ya wanyama ya Katavi. Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa zira hiyo Mh.Josephat Hasunga,wakati akijibu swali la   Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mh.Pudensiana Kikwembe aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu askari wa wanyama pori wanaowanyanyasa wananchi wanaopata huduma ya maji katika mto Kavuu. Akijibu swali hilo,Mh.Hasunga amesema wizara kwa kushirikiana na mbunge pamoja na wananchi watajadili kwa pamoja ili kutatua kero ya maji ambapo kwa sasa wananchi wanahatarisha afya zao kwa kuchota maji katika hifadhi na kukiuka sheria za nchi.

TANESCO SUMBAWANGA YAPOKEA JENERETA YA KUZALISHA UMEME

Image
KITUO cha kufua umeme mkoani Rukwa kimepata jenereta  ya kufua umeme yenye uwezo  wakuzalisha Megawati 10. Akizungumzia ujio wa jenereta hiyo,Meneja wa TANESCO Mkoani Rukwa Bw.Herini Muhina,amesema hali ya uzalishaji umeme itakuwa hivyo bora zaidi na kufanya upatikanaji wa umeme katika wilaya za Sumbawanga Kalambo,Nkasi kuwa bora zaidi pia katika maeneo ya Laela.