KADA MKONGWE WA CHADEMA AFARIKI DUNIA
Mwanasiasa
mkongwe na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tambwe Hizza
amefariki dunia asubuhi ya kuamkia leo (Alhamis ) akiwa nyumbani kwake kwa
ugonjwa wa pumu.
Msemaji
wa Chadema, Tumaini Makene amethibitisha kifo hicho akisema Hiza amefariki leo
asubuhi nyumbani kwake Mbagala akiwa amelala.
Hiza
amefariki kipindi ambacho alikuwa katika timu ya kampeni za kumnadi mgombea wa
ubunge wa Chama hicho katika Jimbo la Kinondoni, Salumu Mwalimu na jana jioni
alipanda jukwaani kumnadi.
Mwaka
2015,Hiza alitangaza kujiunga na Chadema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu
akitokea CCM ambako aliwahi kuhudumu kama mkuu wa kitengo cha propaganda wa
chama hicho tawala.
Kabla
ya kujiunga na CCM alihama kutoka katika Chama cha Wananchi (CUF) ambako pia
alihamia kutoka NCCR-Mageuzi.
Katika kampeni za urais 2015, Hiza alikuwa katika jopo la kumnadi mgombea wa Chadema aliyeungwa mkono na vyama vinavyounda Ukawa,Edward Lowassa na mara zote alikuwa anapanda jukwaani mwanzoni kama alivyokuwa akifanya kwenye kampeni za Mwalimu zinazoendelea.

Habari zaidi
ni P5TANZANIA LIMITED
Comments