TANZANIA KUWA NA WATU 58 MILIONI IFIKAPO MWISHONI MWA 2018
Tanzania
inatarajiwa kufikisha idadi ya watu milioni 58 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu
ikiwa ni ongezeko la juu ikilinganishwa na idadi ya awali ya watu milioni 46
iliyoripotiwa mwaka 2010.
Kwa
mujibu wa Idara ya Jamii na Mambo ya Uchumi ya Shirika la Umoja wa Mataifa
(UN),makadirio hayo ni sawa na kila kilomita moja ya mraba kuna wakazi 67
tofauti na makadirio ya mwaka 2010 ya watu 52.
Inasema
kila sekunde 14,mtoto mmoja anazaliwa nchini huku mtoto mmoja akifariki dunia
kila baada ya sekunde moja.
Makadirio
hayo pia yanaonyesha idadi ya watu nchini imeongezeka kwa asilimia 3.15 kwa
kipindi cha miaka minane iliyopita wakati kiwango cha kuzaliana kilikuwa ni
asilimia 5.17 kati ya mwaka 2015 na 2018.
Ikiwa
hali hiyo itaendelea hivyo,ripoti hiyo inabainisha kuwa idadi ya watu
itaongezeka kufikia milioni 95.5 ifikapo mwaka 2050 na watu milioni 300 ifikapo
mwaka 2099.
Mchanganuo
wa ripoti hiyo unaonyesha kuwa makadirio hayo ni sawa na asilimia 0.77 ya idadi
ya watu duniani kwa mwaka huu kutoka asilimia 0.66 kwa mwaka 2010.
Tanzania
imewekwa katika nafasi ya 24 miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watu
duniani mwaka huu kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na mwaka 2010
ambapo ilikuwa nafasi ya 28.
Idadi
ya hivi sasa ya watu waishio mijini inakadiriwa kufikia milioni 19.2 sawa na
asilimia 31 ya idadi ya watu wote ikilinganishwa na ile ya awali ya mwaka 2010
iliyokuwa milioni 12.6 ambayo ilikuwa sawa na asilimia 27.4.
Hata
hivyo,kulingana na makadirio ya idadi ya watu nchini mwaka 2016-17 yaliyofanywa
na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ilikadiriwa kwamba kungekuwa na idadi ya
watu milioni 51.55 katika kipindi cha mwaka jana.
Habari zaidi
ni P5TANZANIA LIMITED
Comments