KITUO cha kufua umeme mkoani Rukwa kimepata
jenereta ya
kufua umeme yenye uwezo wakuzalisha Megawati 10.
Akizungumzia ujio wa jenereta hiyo,Meneja wa
TANESCO Mkoani Rukwa Bw.Herini Muhina,amesema hali ya uzalishaji umeme itakuwa hivyo
bora zaidi na kufanya upatikanaji wa umeme katika wilaya za Sumbawanga Kalambo,Nkasi
kuwa bora zaidi pia katika maeneo ya Laela.
Kiasi hicho cha Megawati 10
zitakazozalishwa zinaelezwa kuwa zitaimarisha
uzalishaji wa umeme mkoani Rukwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments