SERIKALI KUTATUA KERO YA MAJI VIJIJI VYA JIMBO LA KAVUU
Wizara ya maliasili na utalii inatarajia
kutatua kero ya maji kwa wakazi wa kata ya Itobanilo na vijiji vyake katika Halmashauri
ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi,ili kuondoa mgogoro kati ya askari wa
wanayama pori na wananchi wanaotegemea maji ya mto Kavuu uliopo hifadhi ya taifa
ya wanyama ya Katavi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa
zira hiyo Mh.Josephat Hasunga,wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mh.Pudensiana
Kikwembe aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu askari wa wanyama pori wanaowanyanyasa
wananchi wanaopata huduma ya maji katika mto Kavuu.
Akijibu swali hilo,Mh.Hasunga amesema
wizara kwa kushirikiana na mbunge pamoja na wananchi watajadili kwa pamoja ili kutatua
kero ya maji ambapo kwa sasa wananchi wanahatarisha afya zao kwa kuchota maji
katika hifadhi na kukiuka sheria za nchi.
Mbali na Vijiji vya Sentaunyenye,Senta
Amani na Lunguya katika halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe kutegemea maji kutoka
maeneo ya hifadhi pia wakazi wa kata ya sitalike Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo
nao wamekuwa wakitegemea maji kutoka mto Katuma ambao ni sehemu ya hifadhi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments