HUYU NAYE WIKI HII KADAKWA NA MENO MAWILI YA TEMBO WILAYANI MLELE,MWINGINE NAYE AIBA MPUNGA SHAMBANI AKAMATWA NA WANANCHI ACHOMWA MOTO HADI KIFO.
JUNI 14 mwaka huu,Jeshi la Polisi lilimkamata Oscar Pius Mizengo (30) mkazi wa Kitongoji cha Inyagala - Ikuba Kijiji cha Nyakasi kata ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi akiwa na meno mawili ya tembo yenye uzito wa kilogramu 32 moja likiwa na urefu wa sentimita 150 na lingine 148 cm ambayo thamani yake ni Tsh 30,000,000/= milioni thelasini sawa na tembo mmoja aliyeuwawa.