HUYU NAYE WIKI HII KADAKWA NA MENO MAWILI YA TEMBO WILAYANI MLELE,MWINGINE NAYE AIBA MPUNGA SHAMBANI AKAMATWA NA WANANCHI ACHOMWA MOTO HADI KIFO.
JUNI
14 mwaka huu,Jeshi la Polisi lilimkamata Oscar
Pius Mizengo(30) mkazi wa Kitongoji cha Inyagala - Ikuba Kijiji cha Nyakasi
kata ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi akiwa na meno
mawili ya tembo yenye uzito wa kilogramu 32
moja likiwa na urefu wa sentimita 150
na lingine 148 cm ambayo thamani
yake ni Tsh 30,000,000/= milioni
thelasini sawa na tembo mmoja aliyeuwawa.
Akithibitishwa
kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo,kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ambaye pia ni
mratibu na mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoani SSP Focus Malengo alisema kuwa tukio
hilo lilitokea mnamo Juni 10 mwaka huu katika Kitongoji cha Inyagala - Ikuba
Kijiji cha Nyakasi kata ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
SSP Malengo
alisema Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka kwa raia mwema kuwa mtuhumiwa Oscar
Pius anamiliki meno ya tembo na ndipo ufuatiliaji ulipoanza kwa kufanya upekuzi
katika makazi yake na kufanikiwa kumkamata akiwa na meno hayo huku akiwa
ameyahifadhi shambani kwake kwa kuyafukia chini.
Hata hivyo
mtuhumiwa bado anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano na
anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
Katika
hatua nyingine mwanaume aliyefahamika kwa majina ya Nhuli Nduta anayekadiriwa
kuwa na umri kati ya miaka 53 hadi 40 aliuwawa na kisha mwili wake kuchomwa
moto na watu wasiojulikana kwa tuhuma za wizi wa mpunga ambao haujavunwa shambani.
Aidha,
katika tukio hili Kamanda Malengo alisema hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusika
na mauaji hayo ambapo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji cha
Mnyagala linaendelea na misako mikali kuwabaini na kuwakamata watuhumiwa wa
mauaji hayo.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi alitoa wito
kwa wananchi wanaojihusisha kufanya biashara haramu za magendo kama vile
uharibifu wa rasilimali za Taifa mfano vitendo vya ujangili uwindaji haramu
kuacha mara moja na badala yake wajikite kufanya shughuli halali katika
kujipatia kipato.
Mwandishi :Vumilia
Abel
Mhariri : Issack
Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments