WIKI HII MAMA WA WATU JERA MIEZI SITA KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA GONGO
Mahakama ya wilaya mjini Mpanda
imemhukumu mtu mmoja kifungo cha miezi sita jera au kulipa faini kiasi cha
shilingi laki moja kwa kosa la kukutwa
na pombe haramu.
Akisoma hukumu hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo mh, Chiganga Tengwa
amemtaja mshitakiwa kuwa ni Mariam
Mwanang’ombe (48) mkazi wa Tambukaleli kuwa alitenda kosa hilo mei 31 mwaka
huu asubuhi Nyumbani kwake akiwa na lita 20 za pombe
haramu ya kinyeji aina ya gongo.
Kwa upande wake mshitakiwa alipopewa
nafasi ya kujitetea amaiomba mahakama impunguzie adhabu kwani anaugonjwa wa
kuanguka,ni mjane na anafamilia inayomtegemea.
Hivyo pombe hiyo imeharibiwa na
mahakama imemhukumu ili iwe fundisho kwa
watumiaji na watengenezaji wa pombe haramu.
Mwandishi :Vumilia
Abel
Mhariri : Issack
Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments