WALIMU 16 WAFUTWA KAZINI
JUMLA ya walimu 16 wamefukuzwa kazi wilayani Nkasi mkoani Rukwa kwa kipindi cha miaka mitatu na wengine 11 wamepewa onyo kali baada ya kubainika wametenda makosa mbalimbali. Hatua hiyo imethibitishwa jana na Katibu wa tume ya utumishi wa walimu TSC wilayani humo Richard Katyega mbele ya kamishina wa tume ya Utumishi wa walimu Taifa,Samwel Koroso ambapo alisema kuwa katika kipindi hicho walipokea mashauri 23 na kupelekea walimu 16 kufukuzwa kazi,11 kupewa onyo kali na wengine 5 waliondolewa kazini baada ya kubainika kuwa na vyeti bandia. Alisema katika mwaka wa fedha wa 2016,2017 na 2018 tume hiyo imesikiliza mashauri hayo na kuyatolea maamuzi ambapo ilifikia maamuzi hayo baada ya kusikiliza mashauri hayo na pasipo kumuonea mwalimu hata mmoja na kutenda haki kwa mujibu wa sheria. Katyega alisema tume hiyo sambamba na kuchukua maamuzi hayo pia imekua ikiwahamasisha walimu kufuata maadili ya ualimu kwa uhakika ili wasiweze kukumbana na adhabu mbal...